Wednesday, March 10, 2010

Mwl.MARIJANI


Ni Mwalimu Marijani. Nilipiga nae stori leo kwenye kijiwe kimoja cha mjini-mjini. Mwalimu wetu huyu wa lugha ya Kiingereza aliondoka Tambaza tukiwa Form III mwaka 1986. Alikwenda Jeshi la Polisi. Huko alikwenda kujifunza urubani wa helikopta za polisi. Kwa sasa ni Mkuu wa Idara ya nanihii Mkoa wa Pwani.Nakumbuka siku moja darasani kuna mwenzetu mmoja aliyetokea Tarime ( Jina kapuni) alipandisha jazba na kuleta za kuleta kwa Mwl. Marijani. Naye Mwl. Marijani akatamka huku akikunja shati lake la mikono mirefu; " E bwana hili darasa ni la wanaume watupu. Kama vipi njoo hapa mbele, tuzinanihii..".Form Three 'K' yetu ilikuwa na wenye busara. Tukamsihi jamaa yetu yule mzaliwa wa Tarime atulize jazba yake. Mambo yakaisha. Tumetoka Mbali!

Mtembelee mwanaTambaza mwenzetu kwenye http://www.mjengwa.blogspot.com/

No comments: