Tuesday, May 6, 2008

TAARIFA

“Tazama mbali zaidi”
Simu: 22 2153286/7 /0754317912 SLP: 20576 Dar-Es-Salaam
Barua Pepe:tambsec@yahoo.com/nicolas_buretta@yahoo.com

28 Aprili 2009

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Ndugu Waandishi wa Habari,

YAH: SHULE YA SEKONDARI TAMBAZA KUTIMIZA MIAKA HAMSINI (50)

Shule ya Sekondari ya Tambaza inatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake baadae mwaka huu.Tambaza ni shule yenye historia ndefu na ya kusisimua katika rekodi za kitaaluma nchini Tanzania. Kwa minajili ya kuadhimisha miaka hamsini ya kuanzishwa kwake, Bodi ya shule pamoja na uongozi wa shule umedhamiria kufanya sherehe kubwa ambayo itawashirikisha wanafunzi waliosoma Tambaza na watu waliowahi kufanya kazi Tambaza katika vipindi tofauti. Madhumuni ya kufanya maadhimisho haya ni pamoja na:

Kusherekea jubileI ya miaka 50 ya shule
Kuwakutanisha watu mbalimbali waliosoma na kufanya kazi Tambaza katika vipindi tofauti
Kuhamasisha wanafunzi wa zamani wa Tambaza kuchangia maendeleo ya shule na hivyo kuibua mwamko kwa wananchi kuchangia maendeleo ya shule mbalimbali

Bodi ya shule pamoja na uongozi wa shule utafanya kikao cha maandalizi ya maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 tarehe 11/5/2008 saa nane mchana.Kikao hiki ni cha wazi kwa wanafunzi wote waliowahi kusoma Tambaza. Hivyo kupitia taarifa hii tunawaalika wanafunzi na wafanyakazi wa zamani wa Shule ya sekondari ya Tambaza kushiriki katika kikao hiki.

Historia fupi ya shule ya sekondari Tambaza
Shule ya Sekondari Tambaza ipo katika wilaya ya Ilala mkoa wa Dar-Es-Salaam. Shule hii ilifunguliwa mwishoni mwa mwaka 1957 na shirika la Elimu la Aghakan, ambapo Udaihili wa kwanza ulifanywa mwaka 1958. Shule ilifunguliwa rasmi ikiwa na wanafunzi 117 wa ki-Asia wavulana.Badae shule ilitoa mafunzo ya kidato 1-4 wavulana na kidato cha 5-6 wavulana na wasichana.

Miaka ya 1970 shule ilichukuliwa na serekali na katika kipindi hicho kulikuwa na wanafunzi 273 kidato cha 1-4 wavulama na 5-6 wanafunzi mchanganyiko. Mwaka 1994 shule ilibadilishwa na ikwa inatoa elimu kwa wavulana na wasichana kwa kidato cha 5 na sita tu.

Kwa sasa shule ya sekondari ya Tambaza ina idadi ya wanafunzi 1,000 wavulana kwa wasichana kwenye michepuo 8 ya PCM,PCB,CBG,PGM,EGM,HE,ECA na HKL. Katika kipindi cha miaka hamsini(50) ya kutoa elimu, shule ya sekondari ya Tambaza imefanikiwa kutoa madaktari, mainjinia, marubani, wanasiasa, wahasibu, wachumi, walimu na kada nyingine mbali mbali katika taifa letu.




Wenu katika Maandeleo ya Taaluma


Nicolas James Buretta

Mkuu wa Shule

1 comment:

Anonymous said...

Mr. Buretta tunaomba utupe majina ya wakuu wa shule walioiongoza Tambaza tangia kuanzishwa hadi sasa.

Mdau